Menu

Ni Vipi Kuhusu Wale ambao hawajawahi Kuisikia Injili?

Baadhi ya watu wamehoji haki na upendo wa Mungu kwa misingi ya hukumu Yake juu ya wale ambao hawapati fursa ya kuitii Injili: “Nini kitatokea kwa wale ambao hawajawahi kupewa nafasi ya kumjua Kristo na mafundisho Yake?” Kuna mambo kadhaa yanayostahili kuzingatiwa.

Wanadamu wote wenye umri wa kuwajibika na wenye akili timamu wamefanya dhambi kwa kuvunja amri za Mungu (Warumi 3:9 nakuendelea, 23; 1 Yohana 3:4).Dhambi humuhukumu mtu kwenda jehanamu ya milele,hakuna ubaguzi (Mathayo 10:28; na mengineyo). Njia pekee ya mtu kuepuka athari za dhambi zake ni kusamehewa na Mungu.

Lakini asili ya Uungu ni kwamba Mungu hawezi kupuuza dhambi na kusamehe tu.Kufanya hivyo kungekiuka tabia Yake ya utakatifu usio na mipaka na haki Yake kamilifu. Hivyo, Mungu alilazimika kubuni mpango ambao ungemuwezesha kusamehe dhambi za wanadamu kwa ulinganifu na Uungu Wake. Njia ya pekee na inayostahili ya upatanisho (“upatanisho”—Warumi 3:25; 1 Yohana 2:2) ilikuwa kwa Mungu kuja mwenyewe katika mwili na kujitoa kwa ajili ya dhambi zetu. Alifanya hivyo kupitia kwa Yesu Kristo—Mungu katika mwili. Huu ndio mshangao mkuu wa dhambi usio na mpango wa ukombozi: ndiyo Injili—habari njema kwamba Yesu alifungua njia kwa wanadamu kusamehewa.

Hata hivyo, mpango huo wa ajabu wa wokovu unahitaji mwitikio wa imani yenye utii (Warumi 1:5; 16:26). Mwitikio huo unajumuisha kusikia na kuelewa Injili (Matendo 8:30-32; Warumi 10:17), kuamini Injili hiyo na Yule Anayeitoa (Yohana 8:24; Waebrania 11:6), kutubu dhambi (Matendo 2:38; Luka 13:3), kukiri kwa kinywa uungu wa Kristo (Warumi 10:9-10), na kuzamishwa katika maji ilikuungana na damu ya Kristo kwa ondoleo la dhambi (Warumi 6:3-4; Matendo 22:16).

Kwa kuzingatia ukweli huu wawazi wa kibiblia, dhahiri inapelekea kwamba watu wote wasioungana na damu ya Kristo hawawezi kusamehewa na Mungu. Kwa kweli, Mungu hana uwezo wa kuwasamehe. Kufanya hivyo kungeenda kinyume kabisa na asili Yake—na kwa hivyo, kusingekuwa na uungu—ikiwa Yeye angejaribu kumsamehe mtu kwa msingi mwingine wowote isipokuwa damu ya Kristo. Lakini njia pekee ya kuungana na damu ya Kristo ni kuitii Injili (Warumi 2:5-9). Wale wasioitii Injili watapotelea jehanamu milele (2 Wathesalonike 1:8; 1 Petro 4:17).

Ni dhahiri na inaeleweka kiakili kwamba Mungu hawezi na hatasamehe yeyote ambaye hajabatizwa ndani ya Kristo—kwakuwa hawajaungana na damu ya Kristo, njia ya pekee na  ya kipekee ya upatanisho. Tunapaswa kuhitimisha kwamba hakuna mtu anayeweza kuokolewa bila kuisikia na kuitii Injili (Matendo 4:12). Ikiwa mtu anaweza kuokolewa bila kuisikia na kuitii Injili, basi Yesu asingehitaji kuja duniani na kufa kwa ajili ya dhambi.

Kwa kuzingatia ukweli huu, sasa suala linahama kwenda kwenye swali tofauti: Je, Mungu ni wa haki kwa kuwahukumu watu wote wasiofikiwa na Injili kwendajehanamu? Biblia inatoa jibu  la wazi. Kwanza, wanadamu wote wanaweza na wanapaswa kufikia hitimisho kwamba Mungu yupo kwa kuzingatia ushahidi uliowazi wa Uumbaji wa ajabu unaoonesha uwepo wa Muumba. Baada ya yote,“Hakujiacha pasipo ushuhuda, kwakuwa alitenda mema, akitupatia mvua kutoka mbinguni, na majira yenye kuzaa matunda, akishibisha mioyo yetu kwa chakula na furaha”(Matendo 14:17).

Hakika,“Mbingu zinasimulia utukufu wa Mungu, na anga linatangaza kazi ya mikono yake. Mchana mmoja husemezana na mchana mwingine, na usiku mmoja hutangaza maarifa kwa usiku mwingine. Hakuna lugha wala maneno ambapo sauti yao haisikiki. Urefu wao umeenea duniani pote, na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu”(Zaburi 19:1-4).“Kwa kuwa tangu kuumbwa kwa ulimwengu sifa zake zisizoonekana, yaani, uweza wake wa milele na uungu wake, zinaonekana wazi, zikifahamika kwa yale aliyoyafanya; hata hivyo, wanadamu hawana udhuru”(Warumi 1:20).

Maarifa haya yanapaswa kuwahamasisha watu wote kumtafuta Mungu, kama Paulo alivyowaeleza Waathene:“Ili wamtafute Bwana, kwa matumaini kwamba wangeweza kumtafuta na kumwona, ijapokuwa hayuko  mbali na kila mmoja wetu; kwa maana ndani yake tunaishi, tunakwenda, na tuna uhai wetu”(Matendo 17:27). Katika kumtafuta Mungu, wataweza kuja katika mawasiliano na Ukristo na Biblia:“Wanaonitafuta kwa bidii watanikuta (Mithali 8:17; cf. Mathayo 7:7-8). Kwa wale wenye mioyo ya uaminifu, wema, na unyofu (Luka 8:15), uchunguzi wa Biblia utawafanya kutambua kuwa ndicho kitabu pekee duniani chenye sifa za ufunuo wa kimungu (Yohana 7:17). Hivyo, watajifunza kuhusu Injili na hitaji la kuitii.

Pili, Biblia pia inafundisha kwamba watu wote duniani wenye mioyo inayopokea ukweli watapata fursa ya kuufikia ukweli huo kupitia ulinzi na mpango wa Mungu. Mungu atahakikisha (bila kufanya miujiza yoyote) kwamba wanakutana na Neno Lake. Mungu alimwambia Paulo alipokuwa katika mji wa Korintho, “Nina watu wengi katika mji huu” (Matendo 18:10), alimaanisha kuwa kulikuwa na watu ambao wangepokea ujumbe wa kimungu mara tu watakapoukuta. Hivyo, Paulo alikuwa chombo cha Mungu cha kuwafikia waongofu hao watarajiwa (cf. Matendo 10:4ff.; 16:9ff.).

Uinjilisti wa dunia, yaani, kutangaza Injili katika ulimwengu, ni kazi inayoendelea katika Kanisa. Wakristo wote wanaojitoa kwa mapenzi ya Mungu na walio tayari kutumiwa katika huduma Yake watapata fursa za kuwaathiri watu kwa ukweli. Makusudi ya Mungu hayawezi kuzuiwa. Katika mpango wake wa ajabu wa kimungu katika dunia, Mungu anaweza kuunganisha mioyo inayopokea ukweli na wale watakao watambulisha kwa habari njema (Matendo 8:30; 10:24ff.; Wakolosai 1:23). (Mtandao wa Intaneti umeongeza sana upatikanaji huu wa Injili hata zaidi.) Mungu atahakikisha kuwa wale wenye mioyo inayopokea ukweli wanafikiwa.

Tatu, angalia kwamba wale wote ambao hawatakubali ukweli, hata kama utawasilishwa kwao, hawana haja ya kukutana na ukweli huo, kwa kuwa Mungu anajua kwamba wangeukataa. Hivyo basi, swali “Vipi kuhusu wale ambao hawajawahi kusikia Injili?”linadokeza kwamba kuna watu wasio na hatia na waaminifu ambao wangekubali ukweli ikiwa wangeusikia, lakini hawapati nafasi ya kuusikia. Hakuna watu   wa aina hiyo. Wale wote watakao kubali ukweli wa Mungu  watapewa fursa ya kuupokea kupitia mpango wa Mungu na juhudi zao za dhati za kutafuta ukweli (Mathayo 7:7-8). Wale wote ambao hawajawahi kusikia Injili wasingeikubali hata kama wangepata fursa ya kuisikia.

Nne, na la mwisho, ni kwamba Biblia inafundisha wazi kuwa sehemu kubwa ya wanadamu katika kipindi cha zaidi ya miaka 6,000 ya historia ya dunia hawajapenda ukweli na wasingepokea hata kama ungewafikia (Mathayo 7:13-14; Luka 13:23-24; 1 Wakorintho 1:26; 1 Petro 3:20). Hivyo basi, kazi ya kuwafikishia Injili wale watakaoipokea inapunguzwa kwa kiasi kikubwa. Hakika, njia nyingi zinazotumiwa kufanikisha kazi hii—ikiwa ni pamoja na wamisionari, machapisho, mawasiliano ya ana kwa ana, redio/TV, Intaneti, na nyinginezo—zinafanya iwerahisi kwa wale wenye mioyo inayopokea ukweli kupata fursa ya kuufikia.

Asili ya Mungu ni kwamba lazima awaruhusu  wanadamu wote kutenda kama mawakala wa hiari na kufanya maamuzi yao wenyewe kuhusu hatima yao ya milele. Hivyo basi, Hataingilia uhuru wao wa kuchagua.

Hata hivyo, Mungu amefanya kila awezalo ili kuwawezesha wanadamu kupata ujumbe wa Injili ili wote waweze kusamehewa dhambi na kuishi naye milele. Baada ya yote, Mungu“hutaka watu wote waokolewe, na wafikie ujuzi wa kwelina Yeye“huwa nasi, ili mtu yeyote asipotee, bali wote wasamehewe” (1 Timotheo 2:4; 2 Petro 3:9).


Published

A copied sheet of paper

REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.

Reproduction Stipulations→