Je, Shetani Yupo Kweli?
Q.
Je shetani ni kweli?
A.
Miaka kadhaa iliyopita, baada ya kufundisha darasa la biblia kuhusu kitabu cha mwanzo, Mkristo mmoja wa muda mrefu alinionyesha kwamba haamini kwamba shetani yuko. Bwana huyu alikubali kuwapo kwa wema na uovu, lakini alifikiri kwamba “shetani” lilikuwa neno linalotumiwa katika Maandiko kufafanua uovu, badala ya kurejelea kiumbe mwovu halisi.
Ni kweli kwamba shetani ni mwovu. (Je, umewahi kuona kwamba huwezi kutamka neno “shetani” bila kuandika “uovu”?) kuashiria uovu; yeye ni kama Yesu na Paulo walivyo mrejelea, “yule mwovu” (Mathayo 6:13; 2 Watheselonike 3:3). Yeye si uovu tu; yeye ndiye “yule mwovu” (1 Yohana 3:12). Yeye hawakilishi tu ukosefu wa uaminifu; “Yeye ni mwongo na baba wa huo” (Yohana 8:44).
Ingawa shetani si Mungu na hana kikomo, sifa za milele za Mungu, shetani ni halisi kama Mungu. Yaani, kitabu kile kile kilicho vuviwa na Mungu ambacho kinaeleza juu ya muweza ya yote, mjuzi wa yote, aliye kila mahali, mfadhili wa kila kitu, Muumba mtukufu, pia kinatuambia kuhusu kiumbe halisi wa kiroho aliyeanguka aitwaye shetani. Jina lake linapatikana mara 14 katika sura mbili za kwanza za Ayubu (labda kitabu cha zamani zaidi cha biblia). Maandiko yanafunua kwamba Mungu alikabiliana na shetani katika bustani ya Edeni (Mwanzo 3:14-16). Yesu alizungumza naye nyikani (Mathayo 4:1-11). Na Mikaeli, malaika mkuu akashindana naye juu ya mwili wa Musa (Yuda 9).
Shetani si mhusika wa hadithi sambamba na Mbwa mwitu mkubwa Mbaya au Captain Hook. Yeye si katuni mdogo mwekundu mwenye pembe na uma ambaye anakaa kwa furaha kwenye kiti cha enzi kuzimu (Tazama Butt, 2012). Kadiri wakristo wanavyomchukulia kwa uzito “adui” (shetani), “mshtaki” (Ibilisi), ambaye huenda huku na huko (Ayubu 1:7), “kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze” (1 Petro 5:8), ndivyo tutakavyo kuwa tayari kushinda njama zake (Waefeso 6:11) na mitego (2 Timotheo 2:26). Hatupaswi kumdharau. Yeye si Mungu (na hivyo si mwenye uwezo wote au kujua yote), lakini pia si mtu wa kufikirika. Tofauti na Mungu, anatamani watu wote wapotee (1 Timotheo 2:4). Kwa shukrani “Mungu ni mwaminifu ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili” (1 Wakorintho 10:13).
REJEA
Butt, Kyle (2012). “Satan is Not the Ruler of Hell,”/apPubPage.aspx? pub=1&issue=1026.
REPRODUCTION & DISCLAIMERS: We are happy to grant permission for this article to be reproduced in part or in its entirety, as long as our stipulations are observed.